Friday, 23 February 2018

Haya ndiyo maua ya boga kiboko kwa tiba ya mtoto wa jicho


           Maua ya boga

MTOTO wa jicho ni ugonjwa unaosababisha mboni ya jicho kuwa na alama nyeupe inayozuia uingizaji mwanga ndani yake hivyo kufanya lisitengeneze picha ya vitu vya aina mbalimbali zinazowezesha mtu kuona.

Ugonjwa huu unawapata hasa wenye umri mkubwa (wazee), lakini hata vijana pia wanaweza kuathirika nao.

Tiba ya mtoto wa jicho inaweza kuchukua muda mrefu hivyo mgonjwa awe mvumilivu na makini wakati wa tiba hiyo ambayo ni maua ya boga, asali mbichi, kitunguu swaumu, karoti na paslei.


Maua ya boga

Chukua maua ya boga, tengeneza juisi ambayo utapaka katika kope za macho asubuhi na jioni kwa muda wa mwezi mmoja.

Asali mbichi

Weka matone mawili ya asali katika jicho mara mbili kwa siku kwa muda wa mwezi mmoja hadi miwili.

Kitunguu swaumu

Tafuna taratibu punje tatu za kitunguu swaumu kila siku hadi ugonjwa utakapokuwa umepona.

Karoti

Kila siku hakikisha unatumia robo kilo ya karoti, unaweza kuitumia kwa kutengeneza juisi, kula mbichi au vyote pamoja. Tiba hii endelea nayo hadi mgonjwa atakapo pona.

Paslei (aina ya mboga za majani)

Changanya juisi ya paslei pamoja na ya karoti, kunywa glasi moja ya juisi asubuhi na jioni kwa muda wa mwezi mmoja kila siku. Dawa hizi zimeonesha uwezo mkubwa wa tiba ugonjwa wa mtoto wa jicho.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment