Papai bichi
HEDHI ni
hali ya mwanamke kuona damu yake kila mwezi ambayo inaanza wakati wa kuvunja
ungo (miaka 10 hadi 14) na kukoma katika
umri wa kuanzia miaka 50 na zaidi.
Ni kawaida
kwa mwanamke mjamzito au mwenye umri mkubwa kuacha kuingia katika hedhi.
Hali hii
inapotokea kwa mwanamke yeyote ambaye alishaanza kuingia katika hedhi na hayuko
katika kundi hilo inaashiria kuwa ana tatizo.
Zipo sababu
nyingi zinazopelekea mwanamke kukawia kuingia katika hedhi ambazo ni pamoja na upungufu
wa damu, majonzi, wasiwasi, hofu, matatizo katika sehemu za uzazi na udhaifu wa
mwili.
Zipo tiba
mbalimbali ambazo ni salama zinazoweza kusaidia mtu kuondokana na tatizo hilo ambazo
ni papai, nanasi na ufuta.
Papai
Menya papai
bichi likate vipande vidogo na kula
kiasi cha kikombe kimoja cha vipande hivyo asubuhi na jioni. Endelea na tiba
hii hadi unapoingia katika hedhi.
Nanasi
Katakata
nanasi bichi ambalo bado gumu, kula mchana na jioni hadi utakapoingia katika
hedhi.
Ufuta
Chukua nusu
kijiko cha ufuta uliosagwa tia katika glasi ya maji ya moto, koroga na kunywa
baada ya kupoa. Endelea na tiba hiyo mara mbili kutwa hadi utakapoingia katika
hedhi.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na
Mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.
Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la
kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam
au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali
vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.
Mtaalamu Mandai anapatikana
kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.
No comments:
Post a Comment