Wednesday, 7 February 2018

Hili ndilo suluhisho la kikwapa
KIKWAPA ni harufu inayotoka kwapani kwa binadamu ambayo mara nyingi inakuwa kero kwa watu wanaomzunguka.

Tatizo hili linasababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu  unajitokeza kwapani.

Kimsingi kikwapa cha mtu mmoja kinatofautiana na cha mwingine.

Hata hivyo, tatizo hilo linaweza kutatuliwa kwa njia mbalimbali ambazo ni pamoja na kunywa maji kwa wingi kila siku, wastani wa grasi kati ya sita hadi nane.

Kuoga maji kila siku kutwa mara tatu na kubadili mavazi kila baada ya tendo hilo, kubadilisha nguo zilizoloa jasho kila baada ya kufanya kazi na kula matunda na mboga za majani kwa wingi.

Pia mtu mwenye kikwapa anaweza kutumia juisi ya ndimu iliyochanganywa na ya majani ya beteli kisha apake sehemu za kwapa kila baada ya kuoga na wakati wa kulala. Ukikosa beteli tumia juisi ya limau au ya ndimu pekee.

Jasmini
Tengeneza juisi ya jasmine na kuoshea kwapa mara mbili kutwa na inayobaki itumie kusukutulia kinywa.

Kwa mwenye tatizo hilo na mengine ya kiafya anaweza kuja makao makuu yetu Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Abdallah Mandai kwa ushauri wa namna ya kutumia virutubisho na mimea kukabiliana na changamoto za maradhi mbalimbali.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa +255716 300 200, +255784 300 300, +255769 400 800 au dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufuatilia makala zake kupitia Gazeti TAMBUA kila JUMATATU.

No comments:

Post a Comment