Tuesday, 27 February 2018

Huu ndiyo mchunga kiboko ya tatizo la chunjua

 Mchunga
CHUNJUA ni vinyama vigumu vinavyoweza kujitokeza kwenye ngozi katika sehemu yoyote ya mwili. Kwa kawaida vivimbe hivi vinasababishwa na virusi,  haviumi wala havina madhara kiafya, isipokuwa huleta mwonekano tofauti kwa mtu aliyeathirika navyo.

Tatizo hilo linawapa watu wa rika mbalimbali na wa jinsia zote. Hata hivyo, unapopatwa na tatizo hili usiwe na hofu, zipo dawa asili ambazo ambazo zinasaidia kuondoa tatizo hilo ambazo ni pamoja na chunga, viazi mviringo na kitunguu maji.

Mchunga

Paka utomvu wa mchunga mara tatu kwa siku kwenye sehemu zilizoathirika. Fanya hivyo kwa muda wa wiki mbili utaona mabadiliko makubwa ya tatizo lako.

Viazi mviringo

Chukua kiazi mviringo kimenye kisha kiponde ili kupata uji ambao utautumia kusugua katika chunjua mara tatu kwa siku, kisha endelea na tiba hii kwa muda wa siku 20.

Kitunguu maji

Pia chukua kitunguu maji kiponde kisha paka kwenye chunjua mara tatu kwa siku kwa muda wa siku 20.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kuvurugika hedhi anakaribishwa makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri au kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili ili kuuepusha na magonjwa

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufuatilia makala zake kupitia Gazeti TAMBUA kila JUMATATU.
No comments:

Post a Comment