Friday, 16 February 2018

Ijue nguvu ya bitiruti na chumvi kwa tiba ya shinikizo la chini la damu


TATIZO la shinikizo la chini la damu linasababishwa na kutokula chakula kinachostahili.  Tatizo hili limekuwa likiongezeka kila mara. Shinikizo la chini la damu hujulikana pia kwa lugha ya Kiingereza kama hypotension.

Ni hali ambayo shinikizo la damu ya mtu linakuwa chini sana na kusababisha dalili kama kizunguzungu, uchovu, udhaifu, kupumua kwa shida na kupungua kwa nuru ya macho.
Tatizo hili linaweza kusababishwa na vitu kama kupungua maji mwilini, kulala sana, lishe duni, kushuka kwa wingi wa damu, matatizo ya moyo, ujauzito na homoni kutokuwa sawa.
Baadhi ya dawa za hospitalini pia zinaweza kusababisha tatizo hili. Unaposhughulika na shinikizo la chini la damu inashauriwa kuongeza matumizi ya chumvi na maji.
Hata hivyo, ni vema ukawasiliana na mtaalamu wa afya aliye karibu nawe kabla ya kuamua lolote mwenyewe binafsi. Pia tatizo hilo linaweza kutokea damu inapokuwa imevuja sana, kukata tamaa kwa muda mrefu na kukasirika mara kwa mara.
Kuna njia mbili ambazo ukitumia unaweza kupata nafuu kutokana na tatizo hilo ambazo ni matumizi ya bitiruti na chumvi.

 Bitiruti
Juisi ya bitiruti ni moja ya tiba zinazofaa katika kurekebisha shinikizo la chini la damu.
Mgonjwa  anashauriwa kunywa glasi moja ya juisi ya bitiruti mara mbili kwa siku kwa muda wa siku saba. Hata hivyo, matibabu haya yanaweza kujirudia kulingana na hitaji la mgonjwa.

Chumvi
Mgonjwa atumie chakula chenye chumvi nyingi na kwa nyongeza anywe glasi moja ya maji iliyoongezwa chumvi nusu kijiko cha chai, kila siku hadi atakapokuwa amerudia hali yake ya kawaida. Mgonjwa pia atumie vyakula vyenye protini, vitamin C na B.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.
No comments:

Post a Comment