Tuesday, 6 February 2018

Ijue nguvu ya jivu la kifuu cha nazi katika kupambana na tezi la shingo

                               Mtu aliyeathiriwa na tezi la shingo

UGONJWA wa tezi la shingoni unasababishwa na ukosefu au upungufu wa madini ya ayodini kwenye vifuko vinavyojulikana kitaalam kama 'thyroid glands'.

Licha ya upungufu wa madini hayo, wengine wanaoathiriwa na tatizo hilo ni wale wanaokula vyakula vilivyosindikwa au visivyo vya asili, au wanaokula vyakula ambavyo havipikwi.

Mtu aliyeathiriwa na tezi la shingo anaweza kufahamu iwapo ameathiriwa na tatizo hilo kwa kujiona mwenye kusononeka bila sababu, mwenye kukosa umakini katika mambo mbalimbali, asiye na utulivu wa akili, anavimba vifuko vya thairoidi, pia anakuwa mwenye kutawaliwa na hasira.

Pamoja na tiba nyingine, ulaji kwa wingi wa vyakula vyenye ayodini unasaidia kuondokana na tatizo la tezi la shingoni.

Vitu au vyakula vyenye ayodini ambavyo ukivitumia vinasaidia kupambana na tatizo hilo ni pamoja na mboga aina ya chunga, mchanganyiko wa vyakula, mchicha, majivu ya kifuu cha nazi na tangawizi.

Jivu la kifuu cha nazi
Weka jivu la kifuu cha nazi ndani ya kifuko cha kitambaa, lowanisha na maji kidogo, funga kwenye tezi la shingo usiku mzima, endelea na tiba hii ndani ya siku 10.

Mchicha
Chukua mchicha kiasi, pondaponda, fungia shingoni pale penye uvimbe wakati wa kulala, funga mchicha mpya kila siku ndani ya siku 10.

Tangawizi
Pondaponda tangawizi gramu 20, chemsha ndani ya maji lita kwa muda wa dakika 15 ipua na kunywa kama chai baada ya kuongeza vijiko viwili vya mezani vya asali, endelea na tiba hii katika kipindi cha siku 15.

Chakula mchanganyiko
Kula vyakula ambavyo vina kiasi kikubwa cha ayodini katika milo yako ya kila siku, hakikisha unapata vyakula hivyo kwa wingi. Miongoni mwavyo ni karoti, kitunguu swaumu, kitunguu maji, nanasi, kiini cha yai, mapera, machungwa, ndimu, limau na nyanya.

Mchunga
Pondaponda majani ya mchunga changanya na kiasi kidogo cha samli, chukua mchanganyiko huo ufunge na bandeji kwenye tezi la shingoni. Fanya hivyo kila siku kwa kuweka chunga jipya katika kipindi cha siku 21.
No comments:

Post a Comment