Friday, 16 February 2018

Je, waijua nguvu ya bizari katika kutibu upele?

UPELE ni ugonjwa wa ngozi ambao unasababishwa na ukosefu wa viini vya kutosha katika chakula pamoja na uchafu wa mwili na mazingira yake.

Mgonjwa wa upele anajisikia kuwashwa na kujikuna wakati wote. Upele unaweza kuwa mdogo kama ule wa ugonjwa wa surua au mkubwa kama wa tetekuwanga.

Zipo tiba mbalimbali zinazoweza kutumika kutibu maradhi ya upele ambapo ni pamoja na bizari, karela/ndimu, mnanaa na ndizi.

Bizari
Pondaponda vikonyo viwili au vitatu vya bizari, ongeza maji ya kutosha ili kupata rojo. Baada ya kuoga paka sehemu zote zilizoathirika na upele wakati wa asubuhi na jioni.

Pia  tengeneza glasi moja ya bizari na ongeza kijiko kimoja cha mezani cha asali, kunywa. Endelea na tiba hiyo kwa muda wa siku 10.

Karela/ndimu
Tengeneza juisi ya matunda mawili ya karela, kamulia ndimu moja ndani ya juisi hii, kunywa yote wakati wa asubuhi na jioni kabla ya kula chakula chochote. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku nne.

Mnanaa
Pondaponda mnanaa, ongeza maji ya kutosha, paka sehemu za mwili zilizoathirika kwa upele. Endelea kufanya hivyo katika kipindi cha siku 10, utaona nguvu kubwa ya mnanaa.

Ndizi/muarobaini
Chukua ndizi yenye rangi ya njano iliyowiva vizuri pondaponda changanya na maji ya muarobaini yaliyopatikana kwa kuchemsha majani ya mti huo kisha paka mwili mzima baada ya saa moja oga. Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa siku 10.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya ikiwemo ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.
No comments:

Post a Comment