Tuesday, 20 February 2018

Jiimarisheni kiroho acheni dhambi- KatekistaClaudia Kayombo

WAKATI wakristo wakiendelea na kipindi cha mfungo wa Kwaresma rai imetolewa kwao kujiimarisha kiroho kwa kuacha dhambi.

Katesta Ansgar Mwani wa parokia ya Chanika Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, amewataka kutumia kipindi hiki kufanya toba ili kubaki imara wao na kanisa zima.

Ameyasema hayo Dominika iliyopita wakati akihubiri katika Ibada ya misa ya pili iliyoadhimishwa na paroko msaidizi wa parokia hiyo, Padri Jobi Joseph.

Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Generali Simon Sirro, Katekista Mwani amesema, “tatizo dhambi imetawala, hakuna hofu ya Mungu, tutumie wakati huu kutubu.

“Mwanzo Mungu aliwatumia manabii, sasa amemtuma mwanaye aje kutukomboa, tuitumie Kwaresma kutubu kwa kuwa hatujui siku wala saa.

Kuhusu kuchelewa katika nyumba za ibada au kutohudhuria kabisa ibada za misa takatifu siku za Dominika, alisema ulegevu unapelekea miongoni mwa wakristo kufanya hivyo.

Amefafanua kuwa mkristo anayechelewa kanisani, huyo huyo akiagizwa na daktari kwenda katika matibabu hata kama ni saa 11 alfajiri akitokea nyumbani kwake hachelewi japo hata dakika moja.

“Wakati huu wa Kwaresma Yesu anatuambia tushiriki kitubio, pia tumwombe Mungu tusiwe wakristo wa majina, bali tuyaishi yale tunayotakiwa na Kristo kuyafanya,”amebainisha.

No comments:

Post a Comment