Saturday, 24 February 2018

Kolimba aongoza maadhimisho ya Uhuru wa Kuwait


Dk Suzan Kolimba wa Pili kushoto na washiriki wengine wakizindua maadhimisho hayo

Khamis Musa

NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk. Suzan Kolimba ameongoza wageni mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 57 Uhuru wa Kuwait.

Ubalozi wa Kuwait nchini, umeandaa hafla hiyo ya kuadhimisha miaka 57 ya Uhuru wa Kuwait, mingine 27 ya ukombozi na miaka 12 tangu Mfalme wa Kuwait Sheikh Sabah Al-Ahmad Al-Jaber Al-Sabah apokee uongozi wa nchi hiyo. 

Hafla hiyo imehudhuriwa pia na wageni wengine waalikwa kama, Waziri Mkuu mstaafu Dk. Salim Ahmed Salim, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zubeir Ali Maulid, Mufti wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni, mabalozi wa nchi za kigeni wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, mashirika ya kimataifa na wataalamu wa fani mbalimbali.


No comments:

Post a Comment