Wednesday, 28 February 2018

Korea Kaskazini 'inaisaidia Syria silaha za kemikali'


 Waathiriwa wa gesi ya chlorine nchini Syria
KOREA Kaskazini imekuwa ikiwatumia vifaa Syria ambavyo vinaweza tumika kutengeneza silaha za kemikali, ripoti ya chombo cha habari cha Marekani imesema ikinukuu kutoka ripoti ya Umoja wa Mataifa (UN).
Kwa mujibu wa ripoti ya UN ambayo haijatolewa, wataalam wa bakora Pyongyang wameonekana katika viwanda vya kutengenezea silaha nchini Syria, gazeti la New York Times limesema.
Shutuma hizo zinakuja baada ya ripoti mpya ya utumiwaji wa gesi ya chlorine na vikosi vya Syria, ambayo imekanushwa na serikali ya nchi hiyo.
Korea Kaskazini ipo chini ya vikwazo vya kimataifa sababu ya programu yao ya nuklia.
Vifaa hivyo vinaripotiwa kupatikana kiwizi na kutumwa Syria na Korea Kaskazini vikiwemo vigae venye uwezo wa kuzuia joto na tindikali pamoja na vipima joto.
Vigae vinasemekana kutumika katika kujenga majengo ambayo silaha za kemikali zitatengenezwa. Inasemekana wametumiwa makumi ya mizigo ndani ya miaka kadha.
Gazeti hilo linasema, taasisi ya utafiti ya masuala ya sayansi ya Syria inasemekana kuwa Korea Kaskazini inafanya hivyo kupitia kumpuni bandia.
Serikali ya Syria imeripotiwa kuiambia Umoja wa Mataifa kuwa raia wa Korea Kaskazini waliopo Syria ni makocha na wanariadha tu.
Syria iliungana na mkutano wa silaha za kemikali na kukubali kuteketeza silaha hizo mwaka 2013 baada ya shambulio lililotumia gesi ya sarin na kuwaua mamia ya watu Ghouta.
Tangu mwaka huo, imeshutumiwa kwa kutumia silaha hizo marufuku mara kwa mara katika vita hiyo ya wenyewe kwa wenyewe.


No comments:

Post a Comment