Saturday, 24 February 2018

Kutoona usiku tatizo linalotibiwa kwa mboga za majani na matunda


      Karoti ni moja ya tiba nzuri sana ya tatizo la kutoona usiku

KUTOONA usiku  ni tatizo linaloikaribili jamii kubwa katika nyakati hizi. Kwa bahati mbaya watu wengi hawajui nini chanzo cha tatizo hilo.

Kutokufahamu chanzo kunaiwia vigumu jamii hiyo kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo ambalo wakati mwingine linawapata zaidi watu wenye umri mkubwa licha ya kuwa watu rika zingine wakiwemo watoto na vijana huwakumba pia.

Tafiti za kitabibu zimeonesha kuwa ulaji wa vyakula vyenye ukosefu wa vitamin A katika vyakula vya kila siku unachangia tatizo hilo kwa kiwango kikubwa zaidi.

Hivyo, ili kutibu tatizo hilo ni vema mgonjwa  akala kwa wingi vyakula vinavyochochea vitamin A. Vyakula hivyo ni matunda na mboga za majani kama karoti, spinachi, bitiruti, bamia, embe, tikiti maji, siagi na viazi vitamu.

Pia tatizo hili linaweza kutibiwa kwa muarobaini dawa inayotokana na mimea.

Unaandaa dawa hii kwa kuponda majani yake kisha ongeza maji kidogo,  ichuje na kitambaa safi kisha weka matone mawili ya muarobaini katika kila jicho na inayobaki paka jicho zima kwa ujumla. Tiba hii ifanye kila jioni giza linapoanza kuingia.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment