KUMEKUWA na jitihada mbalimbali za kimatibabu
zinazochukuliwa na jamii punde ndugu au mwanajamii anapoungua moto ili kumtibu
jeraha.
Pamoja na tiba za kisasa mgonjwa anaweza kutibiwa
kwa kutumia vyakula na mimea mingine yenye uwezo mkubwa wa uponyaji.
Tiba hizo ni pamoja na ndizi mbivu, mchele, ufuta,
ndimu, chumvi, asali na muarobaini.
Ndizi mbivu
Ponda ndizi iliyowiva vizuri paka katika sehemu
iliyoungua halafu bandika jani la mgomba kama bandeji. Endelea kufanya hivyo
hadi kidonda kipone.
Mchele
Nyunyiza unga wa mchele katika sehemu zote
zilizoungua, unaweza kunyunyizia pia unga wa mhogo kila baada ya kuoga. Endelea
na tiba hii hadi utakapo pona.
Ufuta na ndimu
Chukua mafuta ya ufuta, changanya na maji ya ndimu
kiasi sawa paka sehemu iliyoungua, endelea kufanya hivyo kila baada ya kuosha
kidonda hadi kitakapo pona.
Chumvi na ndizi
Baada ya kuungua nyunyiza chumvi sehemu yote
iliyoungua, baada ya dakika kumi na tano paka ndizi mbivu iliyopondwa.
Asali
Paka asali kwenye sehemu yote iliyoungua, endelea
kufanya hivyo kila siku hadi kidonda kitakapo pona.
Muarobaini
Chukua majani ya muarobaini, changanya na mafuta ya
karanga au ufuta bandika kwenye sehemu iliyoungua. Endelea na tiba hii hadi
utakapo pona.
Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho,
Abdallah Mandai.
Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao
yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai
kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya
magonjwa.
Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au
barua pepe dkmandaitz@gmail.com.
No comments:
Post a Comment