Monday, 5 February 2018

Maandamano kushinikiza kufunguliwa televisheni kufanyika leoWAHARAKATI nchini Kenya wamepanga kufanya maandamano makubwa ili kuishinikiza Serikali ya nchi hiyo kuvifungua vyombo vitatu vya habari vilivyozuiwa kuendelea na matangazo yake ikiwa leo ni siku ya saba.

Serikali ilizifunga stesheni tatu za televisheni NTV, Citizen na KTN kwa madai kuwa zilipanga njama za kupeperusha moja kwa moja  matangazo ya kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama rais licha ya onyo iliyotoa.

Sasa makundi ya kutetea haki za binadamu, waandishi habari na baadhi ya wananchi wanapanga kufanya maadamano leo katika jiji la Nairobi kuishinikiza serikali kutii amri ya mahakama.

Waandalizi wa maandamano hayo wanaishtumu serikali wakidai imekiuka haki za kibinadamu, kuendeleza mashambulizi dhidi ya vyombo vya habari kando na kupunguza uhuru wa demokrasia nchini kwa kutoheshimu katiba.


No comments:

Post a Comment