Friday, 2 February 2018

Madondo kirutubisho chenye nguvu ya kupambana na kiharusi


Kirutubisho Madondo Plus E6
UGONJWA wa kiharusi au 'stroke' unatokea kwa mtu baada ya sehemu ya ubongo wake kushindwa kupata mzunguko wa damu na hivyo chembe hai kufa kwa kukosa hewa safi na virutubisho vingine vinavyohitajika na ogani hiyo.

Kimsingi Kiharusi ni hali ya dharura inayompata mtu na hivyo kuhitaji matibabu ya haraka  yaliyo makini.  Tafiti za kitabibu zinaonesha kuwa takriban watu milioni 17 duniani walipata kiharusi mwaka 2010 na wengine milioni 33 walikuwa wamepata matatizo hayo awali.

Kati ya mwaka 1990 na 2010, idadi ya visa vya kiharusi vinavyotokea kila mwaka duniani vilipungua kwa takriban asilimia 10 kwenye mataifa yaliyostawi na kuongezeka kwa asilimia 10 katika mataifa yanayostawi. Mwaka wa 2013, kiharusi kilikuwa cha pili kusababisha vifo baada ya ugonjwa wa shinikizo la moyo.

Dalili za kiharusi

Mwili kupata ganzi au udhaifu, mara nyingi hali hiyo huanza ghafla ambapo hutokea upande mmoja wa mwili kushoto au kulia au upande mmoja wa uso kupata ganzi au kuwa dhaifu.

Pia mtu anaweza kujikuta ghafla anashindwa kuona au kitu kimoja vinaonekana viwili ua wakati mwingine kuona ukungu badala ya kitu halisi, hali hiyo inaweza kutokea kwa jicho moja au yote mawili.

Mtu alikumbwa na kiharusi anaweza kuona maumivu makali ya kichwa bila sababu wakati mwingine hali hiyo inaambatana na kichefuchefu.
Kuzuia kiharusi

Matatizo ya kiharusi yanaweza kuzuilika kwa kuangalia au kupima msukumo wa damu mara kwa mara, ni muhimu kwa watu wenye matatizo hayo kuhakikisha damu yao inakuwa katika hali ya kawaida.

Wingi wa lehemu (cholesterol),ambayo inakaa katika mishipa ya binadamu unasababisha kupungua tundu la kupitisha damu ndani ya mishipa yake, hivyo ni vema kupunguza kula vyakula hususan vyenye mafuta mengi kwa kuwa vinavyochangia tatizo hilo.

Uvutaji sigara na unywaji pombe unachangia tatizo hilo kwa kiwango kikubwa hivyo ni vema wavutaji na wanaotumia kilevi wakapunguza au kuacha kabisa.

Mtu mwenye mawazo mengi mwili wake unatengeneza homoni zinazosababisha kuongezeka msukumo wa damu, jamii iepuke mawazo ili kuepuka tatizo hilo.

Tiba ya kiharusi

Kampuni yetu ya virutubisho tiba (Mandai Products Company) imegundua tiba lishe Madondo Plus E6 inayotengenezwa kwa mchanganyiko maalum wa mime ambayo kazi yake kubwa ni kuondoa maumivu mwilini, ganzi na miguu kuwaka moto.

Madondo Plus E6 pia inasaidia ubongo kufanya kazi vizuri kwa kurudisha kumbukumbu, kuongeza hamu ya kula chakula na kumfanya mtumiaji kuwa mchangamfu muda wote.

Kirutubisho hiki husaidi kuondoa maumivu ya mgongo, kiuno, kifua, viungo vya mwili na homa ya mifupa. Ndani ya tiba lishe hii kuna madini ya calcium kwa wingi ambayo ni muhimu katika kuondoa uchovu wa mwili na kuimarisha viungo regevu kwa watoto.

Kwa mwenye tatizo hilo anaweza kuja makao makuu yetu Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Abdallah Mandai kwa ushauri au kujipatia dawa hii.

Pia unaweza kuwasiliana na Mtaalamu Mandai kwa simu +255716 300 200, +255784 300 300, +255769 400 800 au dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufuatilia makala zake kupitia Gazeti TAMBUA kila JUMATATU.

No comments:

Post a Comment