Friday, 2 February 2018

Magufuli ampa shavu Kilagi


RAIS Dk. John Magufuli amemteua Dk. Adelardus Kilagi kuwa Mwanasheria Mkuu mpya wa Tanzania na Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria.

Kabla ya utezi huo, nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa  na George Masaju hadi jana. Rais Magufuli amemwondoa katika nafasi hiyo Masaju na kumteua kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Masaju aliyeshikilia nafasi hiyo kwa muda wa miaka mitatu, aliteuliwa kushika wadhifa huo Januari 2, mwaka 2015 na Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete.

Kabla ya uteuzi huo Dk. Kilangi, alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino, kituo cha Arusha, na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za mkondo wa juu ya mafuta-PURA huku Paul Ngwembe, akiwa Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini.

No comments:

Post a Comment