Tuesday, 27 February 2018

Mapigano yasitishwa kwa muda Syria


 Ramani inayoonesha maeneo yaliyochukuliwa na waasi huko Syria
 RAIS wa Urusi, Vladmir Putin ameagiza usitishwaji wa mapigano kwa takriban saa tano katika mashambulizi yanayofanywa na serikali ya Syria katika maeneo ya mashariki mwa eneo la Ghouta linalodhibitiwa na waasi.
Usitishwaji huo wa mapigano unaanza leo Jumanne na utajumuisha kuundwa kwa kile kinachoitwa '' Njia ya Hisani'' kuwawezesha raia kuondoka katika eneo hilo lenye mapigano makali.
Waziri wa Ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu ametoa tangazo kuhusu kusitishwa huko kwa mapigano, kwa kusema kuwa litaanza kati ya saa tatu mpaka saa nane kwa saa za eneo la tukio ama saa moja mpaka saa sita GMT, kila siku.
Taarifa zaidi iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema Shirika la Msalaba mwekundu la Syria litasaidia mpango huo wa uokozi na kwamba watu watapewa taarifa kupitia vipeperushi, ujumbe wa simu na video.
Waasi wanaopigana, wamezingirwa karibu na mji mkuu wa Damascus, ambako raia 393,000, wamekwama, huku mashambulizi makali yakifanywa na majeshi ya serikali yanayoungwa mkono na Urusi.
Kwa mujibu ya makundi ya waangalizi, zaidi ya watu 560 wameuawa katika siku nane za mapambano.
BBCNo comments:

Post a Comment