Monday, 12 February 2018

Mbunge Chadema aijia juu Serikali
MBUNGE wa Viti Maalum, Joyce Sokombi (Chadema), amemshukia Naibu Waziri wa  Mifugo na Uvuvi, Abdaallah Ulega kwa kile alichodai ameshindwa kujibu kwa ufasaha maswali yake ya msingi.

Sokombi ametoa kauli hiyo bungeni Ijumaa siku ambayo Bunge lilikuwa linaahirishwa, wakati wa kipindi cha maswali na majibu, alipokuwa akiuliza swali la nyongeza.

Mbunge huyo amesema majibu ya serikali aliyojibiwa katika swali lake la msingi hayana ukweli na kwamba waliomwandalia majibu wamempotosha.

Katika swali la nyongeza mbunge huyo alitaka kujua serikali inatenganishaje uvuaji wa samaki wadogo na wakubwa kwa mfano wa samaki kama gogo, furu na nembe.

Aidha, alitaka kujua serikali inatoa tamko gani kwa wavuvi ambao wanakamatwa wakiwa na samaki wadogo.

Mbali na hilo alitaka kusikia kauli ya serikali ni kwanini imekuwa ikiwanyanyasa wavuvi wa Tanzania wakati wavuvi wa nchi za jirani wanavua bila usumbufu.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni nyavu zenye ukubwa gani zinahitajika kwa ajili ya uvuvi wa samaki wadogo.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema zipo nyavu sahihi zinazotakiwa kutumiwa kwa kuzingatia na sheria.

Joyce SokombiNo comments:

Post a Comment