Saturday, 24 February 2018

Milioni 80 zatumika kuendeleza kijiji


 Mkuu wa wilaya ya Kilosa, Adam Mgoi akioneshwa ramani ya nanma wanakiji wa wanavovuna mkaa endelevu na mwenyekiti wa wazalishaji mkaa endelevu kijiji cha Ulaya, Rashid Kazeuka alipotembelea msitu unaotunzwa na wanakijiji wa kijiji hicho (PICHA NA SULEIMAN KASEI).Suleiman Kasei, Kilosa

KAMATI ya Maliasili ya Kijiji cha Ulaya Mbuyuni, wilayani Kilosa, mkoani Morogoro imetoa zaidi ya sh. milioni 80 kwa ajili ya maendeleo ya kijiji katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2018.

Hayo yamebainishwa na Katibu wa kamati hiyo, Victoria Ndekelo wakati akiwasilisha ripoti ya kijiji kuhusu Mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS), mbele ya mkuu wa wilaya hiyo, Adam Mgoi ambaye alitembelea kijiji hicho kuangalia utekelezaji wa mradi huo.

Mradi huo wa TTCS unatekelezwa na Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (Mjumita) na Shirika la Kuendeleza Nishati Tanzania (TaTEDO) kwa  ufadhili Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswiss  (SDC).


No comments:

Post a Comment