Saturday, 10 February 2018

Mkakati uzalishaji viwanja watekelezwa


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Joyce Kasiki, Dodoma


HALMASHAURI ya manispaa ya Dodoma inatekeleza mkakati wake wa kuzalisha viwanja 30,000 ili kukabiliana na changamoto ya mahitaji ya viwanja baada ya agizo la Serikali la kuhamishia makao makuu ya nchi mkoani hapa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ametoa kauli hiyo  mjini hapa wakati akiahirisha mkutano wa 10 wa Bunge.

Majaliwa amesema mahitaji ya viwanja hadi Februari yalikuwa  ni viwanja 24,602, amefafanua kuwa viwanja vipya vilivyopimwa hadi sasa ni 15,316 .

Kwa mujibu wa Majaliwa, viwanja hivyo vitaanza kugawiwa kwa waombaji kuanzia Machi 30, mwaka huu huku akisema kiasi kilichobaki cha viwanja 14,684 ,kitakamilika ifikapo Juni, 2018.

Ametoa mwito kwa watumishi wa umma watakaohitaji viwanja kufuata taratibu za maombi ya viwanja pindi vitakapotangazwa rasmi.

Vile vile alizungumzia kuhusu mchakato wa kubadilisha hati zilizotolewa na iliyokuwa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) na kupata hati miliki za miaka 99 ambapo amesema mchakato huo unaendelea .

Amewasisitiza wananchi wenye hati za CDA kuendelea na taratibu za kubadilisha kupata zile za manispaa.


No comments:

Post a Comment