Friday, 23 February 2018

Mnyika ataka viongozi Chadema kujilinda dhidi ya wauaji

                  John Mnyika


KAIMU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amesema mauaji ya kutisha yanayotokea nchini yanatisha hivyo amewataka viongozi wa chama hicho na Watanzania kwa ujumla kuchukua tahadhari.

Mnyika ambaye pia ni mbunge wa Kibamba ametoa kauli hiyo leo, Dar es Salaam, wakati akizungumza na wanahabari huku akitoa mwito kwa viongozi wa chama hicho kuchukua tahadhari kubwa baada ya vifo vingi kutokea siku za hivi karibuni kuwa ni vya viongozi wa Chadema.

“Mfululizo wa matukio ya viongozi wa Chadema kuuawa, kumtesa na kumuua  katibu wa chama chetu kata ya Hananasifu Dar es Salaam, Daniel John;  Godfrey Luena ambaye ambaye tumeelezwa baada ya kukatika umeme  alipotoka,  akashambuliwa na kuuawa usiku wa kuamkia leo.

“Katika mazingira kama haya, tunatoa mwito kwa viongozi wa Chadema nchi nzima,  kwa wabunge na madiwani kuchukua tahadhari kubwa na kujilinda.

“Mambo haya yamefikia kwa wanahabari, Azory Gwanda wa Mwananchi  hadi sasa hajulikani alipo,  na Emmanuel Kibiki wa Raia Mwema wa Makambako Njombe ambaye naye alikamatwa. Hizi ni ishara kwamba katika taifa letu kuna vikundi vya watekaji, watesaji na wauaji,” amesema.No comments:

Post a Comment