Monday, 26 February 2018

Moto wateketeza hospitali ya Aga Khani Dodoma

MOTO mkubwa umezuka katika jengo la Hospital ya Aga Khani (Apolo Medical Centre) mkoani hapa na kuteketeza baadhi ya mali huku chanzo kikielezwa kuwa ni hitilafu ya umeme.

Akizungumza baada ya kuzimwa moto huo, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la zima moto na uokoaji mkoani Dodoma, Regina Kaombwe amesema walipokea taarifa za moto huo jana saa kumi na moja kasorobo jioni ambapo waliwahi
eneo la tukio na kukuta jengo lote likiwa linawaka moto hivyo walifanikiwa kuudhibiti .

Amesema jitihada  kubwa waliyoifanya ni  kuhakikisha moto
huo hauenei maeneo mengine hususan benk ya NMB ambayo ipo karibu na hospitali hiyo na walifanikiwa katika hilo.

Nao baadhi ya wafanyakazi katika hospital hiyo wamezungumzia tukio hilo huku wakilishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kuwahi eneo la tukio licha ya kuwa vitu vingi viliteketea kutokana na moto.

Wametaja vitu vilivyoteketea  kuwa ni pamoja na mashine ya xray, kompyuta na vitanda vya wagonwa wakati mwa vichache vilivyookolewa ni mafaili na mabenchi ya kukalia

Hadi sasa haijajulikana thamani ya vitu vilivyoteketea huku jeshi hilo likitoa mwito kwa wananchi pindi wanapoona matukio ya moto  watoe taarifa mapema kwa kupiga simu namba 114 kwa ajili ya uokoaji wa haraka.No comments:

Post a Comment