Monday, 19 February 2018

Msafara wa Rais Kabila wakumbwa na ajali nyingine


Rais Joseph Kabila


MSAFARA wa magari ya Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo DRC, Joseph Kabila yamehusika kwenye ajali nyingine ya barabarani akiwa nchini Zambia.
Ajali hiyo ilitokea wakati msafara wake ulikuwa ukielekea makao ya rais wa zamani Keneth Kaunda eneo la Lusaka East.
Gari dogo liligonga jingine lililokuwa kwenye msafara wa rais ambapo Rais Kabila na waziri wa mashauri ya nchi za kigeni, Joe Malanji walikuwa, kwenye barabara ya Leopards eneo la Woodlands.
Wote hawakujeruhiwa. Ripoti za awali zilisema kuwa Rais Edgar Lungu alikuwa kwenye gari lililopata ajali lakini zilikanwa na ikulu ya rais.
Hii ndiyo ajali ya pili ya barabarani kumkumba Kabila ndani ya wiki moja.
Wiki iliyopitangulia watu watano waliuawa wakati lori dogo lilipogonga msafara wa rais nchini DRC.
Ripoti zilisema kuwa wanajeshi watatu na raia wawili waliuawa kwenye ajali hiyo na watu wengine 11 wakajeruhiwa.
Chanzo BBC

No comments:

Post a Comment