Thursday, 22 February 2018

Mtangazaji wa redio Marekani ajifungua akiwa katika kipindi


                 Cassiday Proctor
MTANGAZAJI  wa redio nchini Marekani, Cassiday Proctor amejifungua akiwa hewani wakati wa kipindi chake cha alfajiri.

Mtangazaji huyo wa kipindi cha redio cha alfajiri katika kituo cha The Arch katika mji wa St Louis nchini Marekani, alitangaza kujifungua kwake kupitia njia ya upasuaji siku ya Jumanne.
Proctor alianza kuhisi uchungu wa kujifungua siku ya Jumatatu, Kituo chake cha habari kilishirikiana na hospitali ambayo alijifungua ili matangazo yake kwenda moja kwa moja hewani.
Ameliambia Shirika la Utangaji BBC kwamba alipata fursa ya kwenda hewani moja kwa moja alipokuwa akijifungua mtoto huyo wiki mbili kabla ya muda uliotarajiwa.
''Ilikuwa furaha kuweza kuwa hewani na wasilikizaji wetu katika siku muhimu ya maisha yangu'' , amesema Proctor kuhusu kipindi hicho.
Amefafanua kuwa kujifungua ukiwa hewani ni mwendelezo wa kile kinachoendelea kila siku katika kipindi hicho ,''mimi huwaambia watazamaji wangu kila kitu kinachoendelea katika maisha yangu.'' .
Mtoto huyo aliyekuwa na uzani wa 7lbs 6oz amepatiwa jina Jameson baada ya wasikilizaji kupendekeza jina la mtoto huyo katika shindano mwezi Januari.
Majina 12 ya kijinga pamoja na mengine 12 yaliochaguliwa na mtangazaji huyo na mumewe yaliwekwa katika sehemu moja .
''Tulipiga kura hadi tulipopata Jameson'', amesema mkurugenzi wa vipindi Scott Roddy .
Mtangazaji mwenza wa Proctor Spencer Graves ameambia BBC kwamba hatua hiyo ya kujifungua hewani ilikuwa ya kipekee. Proctor sasa atakwenda likizo ya uzazi.No comments:

Post a Comment