Wednesday, 21 February 2018

Mvua, upepo vyaleta taflani Namtumbo


Moja ya nyumba zilizoathiriwa na mvua hiyo

Yeremias Ngerangra, Namtumbo

MVUA iliyoambatana na upepo mkali vimeeleta tafrani katika kijiji cha Njalamatata, kata ya Mkongo Nakawale, wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.

Tafrani  hiyo ilitokea siku ya  Jumatatu  wiki hii  baada ya nyumba tano kuezuliwa na upepo na wananchi waliokumbwa na dhahama hiyo kubaki wakihifadhiwa na majirani zao

Katibu Tawala wa Wilaya ya Namtumbo, Adelin Nchimbi akiwa na kamati ya ulinzi na usalama wamekwenda eneo la tukio na kuzungumza na waathirika. 

Kamati ya ulinzi na usalama ikiwa na miongoni mwa waathiriwa wa tukio hilo.

Nchimbi amesema tukio hilo limesababisha nyumba tano kuezuliwa ambapo hakuna mtu aliyepoteza maisha au kujeruhiwa.

Ametaja familia zilizoathirika na mvua hizo kuwa ni  Clavery Ponera ,Donatus Kapinga,James Mdagi ,Sadiki Kapinga ,Rusti  Kimbili na Lotary Hongo wote ni wakazi wa kijiji hicho.

Kamati  ya ulinzi na usalama  ya wilaya ya Namtumbo pamoja  na kutoa pole kwa waathiriwa hao ilifanya mahojiano nao na kubaini hasara iliyopatikana  kutokana na tukio hilo.

Kamati hiyo pia imewashauri wananchi wa kijiji hicho kujenga nyumba na kuziezeka kwa kuweka tengo za kushikizia kwenye ukuta baada ya kubaini baadhi ya nyumba hazijawekwa tengo hizo.
No comments:

Post a Comment