Saturday, 24 February 2018

Mwanamke atumia mbegu za kiume za mwanawe aliyefariki kupata wajukuu


 Rajashree Patil akiketi karibu na picha ya mwanawe aliyefariki kutokana na saratani ya ubongo
MWANAMKE Rajashree Patil, miaka miwili ilioipita, alipoteza mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 27, aliyefariki kwa kuugua saratani ya ubongo.
Huku akipata changamoto za kuishi bila mwanawe, Rajashree alitumia shahawa (mbegu za kiume) za mwanawe huyo ambaye alikuwa hajaoa kumpachika mimba mwanamke mwingine.
Hatua hiyo ilifanikiwa na mama aliyepaichikwa mimba hiyo akajifungua pacha. Rajshree amempa mmoja wa pacha hao jina la mwanawe.
Hiki ni kisa kisichokuwa cha kawaida cha mwalimu mwenye umri wa miaka 49 kutoka India ambaye alikabiliana na changamoto za kila aina ili kutomsahau mwanawe aliyefariki akiwa na umri wa miaka 27 kutokana na saratani.
Akisaidiwa na mama aliyekubali kupachikwa mimba hiyo kwa lengo la kulipwa,  alifanikiwa kupata watoto wawili mmoja akiwa mvulana na mwingine msichana.
Anasema ni njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa mwanawe anaishi. Baada ya kufuzu kutoka chuo cha uhandisi cha Sinhgad mjini Pune, Mwanawe Rajshree Prathamesh alielekea mjini Ujerumani 2010 kusomea shahada.
Mwaka 2013, alipatikana na uvimbe wa ubongo na kufariki 2016 lakini mbegu zake za kiume zilihifadhiwa na baadaye kutumika kumpachika mama wa mimba za biashara aliyejifungua pacha hao.
''Nimempata mwanangu Pramesh'', mamake Rajashree Patil aliambia BBC.
''Nilimpenda sana mwanangu, alikuwa mwerevu sana shuleni na alikuwa akisomea shahada katika uhandisi nchini UJerumani alipopatikana na uvimbe huo ikiwa ni awamu ya nne ya saratani katika ubongo.
Madaktari walikuwa wamemwambia Pramesh kuhifadhi shahawa yake kabla ya kuanza matibabu ya kutumia kemikali na miale, alisema.
Prathamesh ambaye alikuwa hajaoa alikuwa amemchagua mamake na dadake Dnyanashree kutumia shahawa hiyo baada ya kifo chake.
Wakati huo Rajshree hakubaini kwamba hiyo itakuwa njia ya kumpata mwanawe.
Shahawa hizo zilihifadhiwa ilichanganywa na yai ambalo halijaulikani mwenyewe na kupachikwa kwa kizazi cha mwanamke anayefanya biashara ya kukuza mimba.
Baada ya mwanawe mwenye umri wa miaka 27 kufariki kutokana na saratani ya ubongo miaka miwili iliopita, Rajshree alikataa kuomboleza na badala yake alitumia shahawa hiyo ya mwanawe kupata wajukuu hao.
Pacha hao walizaliwa februari 12 na Rajshree aliwapatia majina ya Prathamesh baada ya jia la mwanawe na Preesha (zawadi ya mungu).
   Pacha Prathamesh na Preesha
Huku akisukumwa na lengo la kumpata mwanawe, Dk. Supriya Puranik, ambaye ni mtaalamu wa IVF katika hospitali ya Sahyadri alisema mbinu ya IVF ilikuwa kitu cha kawaida lakini kisa hiki kilikuwa cha kipekee kwa kuwa mama aliyekuwa na huzuni alitaka kumpata mwanawe kwa gharama yoyote ile.
Chanzo BBC


No comments:

Post a Comment