Wednesday, 28 February 2018

Mwimbaji Misri afungwa kwa kuukashifu mto Nile


Mwimbaji maarufu wa Misri Sherine Wahab

MWIMBAJI wa Misri, Sherine Abdel Wahab amehukumiwa kutumia adhabu ya miezi sita gerezani kwa kutania kuwa hali ya usafi wa mto Nile si kuridhisha.
Sherine, ni mmoja wa waimbaji maarufu nchini humo pia ni jaji katika kipindi cha mashindano ya waimbaji, The Voice- alimwambia shabiki wake kuwa kunywa maji kutoka mto huo kunaweza kumpatia vijidudu. "Kunywa Evian badala yake." akatania
Mwimbaji mwingine, Laila Amer, pia alihukumiwa siku ya Jummane kifungo cha miaka miwili kutokana na video ya muziki.
Laila ambaye hana umaarufu kama Sherine - alipatwa na hatia ya 'kuchochea ufitini na uovu". Muongozaji wa kipindi na muigizaji walihukumiwa kwa vipindi vifupi.
Sherine, amehukumiwa na mahakama moja mjini Cairo kwa kusambaza habari zisizo za kweli. Chombo cha habari Misri, Ahram kimesema aliagizwa kulipa paundi 5,000 za Misri.

Mzaha
Mashtaka dhidi ya Sherine yalifunguliwa mwezi Novemba, baada ya kuonekana video mtandaoni ikimuonesha akiombwa kuimba wimbo uitwao Mashrebtesh Men Nilha (umewahi kunywa maji ya mto Nile?).akajibu ''Nikinywa maji ya mto Nile nitapata kichocho''. Kichocho ni ugonjwa unaojitokeza maeneo ya vijijini nchini Misri.
Mbali na kesi dhidi yake, Chama cha wanamuziki nchini humo kimetangaza kuwa kimempiga marufuku kuuimba wimbo huo kuhusu Misri.
Abdel Wahab baadaye aliomba radhi kutokana na tukio hilo akiwa kwenye tamasha lililofanyika huko Jumuia ya falme za kiarabu zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Uamuzi wa mahakama uliotolewa siku ya Jumanne unafanya idadi ya wanamuziki kuhukumiwa kifungo kufikia watatu miezi ya hivi karibuni
Mwezi Desemba, Shaimaa Ahmed ajulikanaye kifupi Shyma alihukumiwa kifungo cha miaka miwili baada ya kuonekana kwenye video ya muziki akiwa amevalia nguo za ndani huku akila ndizi kwa mbwembwe.
Alikutwa na hatia ya kuweka video yenye maadili mabaya akahukumiwa pamoja na muongozaji wa video hiyo. Baadaye hukumu ilipunguzwa na kuwa ya mwaka mmoja baada ya kukata rufaa.


No comments:

Post a Comment