Thursday, 15 February 2018

Ndejembi akuna kichwa kuinusuru elimu Dodoma
    Deo Ndejembi

Joyce Kasiki, Dodoma
KAIMU mkuu wa wilaya ya Dodoma, Deo Ndejembi amesema hali ya elimu wilayani hapa siyo nzuri hivyo amewataka wadau kubuni mbinu mpya zitakatatua tatizo hilo.

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha wadau wa elimu kilichoketi kwa ajili ya kuangalia changamoto na kuzitatua katika sekta ya elimu.

Amebainisha kuwa Dodoma ni makao makuu ya nchi na wageni wengi sasa wanahamia hapa hivyo itakuwa ni aibu kwa wilaya kuwa na matokeo mabaya katika sekya hiyo.

Amewataka wadau hao kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hiyo na kuifutilia utekelezaji wake badala ya kutoka na mikakati hiyo na kisha kuifungia makabatini.

 “Wilaya yetu ndiyo wilaya ya Makao Mkuu ya nchi na elimu yetu inatakiwa ‘ireflect’ na ujio wa makao makuu, lazima tuhakikishe tunaweka mikakati ya kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda katika wilaya yetu,” amesema Ndejembi.

Ametaka kikao hicho kitumie watu wenye uzoefu wanaoweza kusaidia kupandisha kiwango cha ufaulu.


No comments:

Post a Comment