Wednesday, 21 February 2018

Njia tano unazoweza kutumia kuzuia kuota mvi, kunyonyoka nywele


KWA kawaida katika mwili wa binadamu licha ya nywele kufunika kichwa chake pia vinyweleo vimemzunguka mwili mzima.  Nywele pamoja na sifa nyingine zinamwongezea unadhifu binadamu


Wakati nywele zikitajwa kumwongezea binadamu unadhifu, baadhi ya watu wamejikuta wakikumbwa na matatizo ya kunyonyoka au kuota mvi wakingali vijana.


Hivyo, zipo tiba mbalimbali zinazosaidia waathirika kuondokana na matatizo hayo. Baadhi ni matumizi ya ufuta, ndimu, tui la nazi, mbegu za ndimu, jino la tembo na mafuta ya nazi.


Ufuta


Ponda pamoja majani na mizizi ya ufuta kisha vichemshe na maji, halafu vichuje maji yake oshea kichwa chako na kukisuuza kwa maji hayo kila unapomaliza kuoga.

Hii inasaidia kuondoa mba kichwani, kukawia kuota mvi na kukuza nywele. Tumia dawa hii kwa muda wa mwezi mmoja.


Ndimu


Baada ya kuosha nywele zako vizuri suuza kwa kutumia mchanganyiko wa kijiko kimoja cha mezani cha maji ya ndimu na glasi moja ya maji ya kawaida. Hii ni tiba kwa ajili ya mba na kufanya nwele zikue haraka.

Tui la nazi


Baada ya kuosha nywele zako vizuri, malizia na tui la nazi lililochujwa vizuri, hakikisha tui linaingia hadi katika vishina vya nywele. Hii ni pia tiba kwa ajili ya mba na kufanya nywele zikue haraka.


Mbegu za ndimu


Chukua mbegu za ndimu na pilipili manga kwa kiasi kinacholingana, viponde pamoja ili kupata mchangayiko mzuri, ongeza maji ya tangawizi kisha paka mchanyiko huo kichwani kila siku jioni. Tiba hii inasaidia kuotesha nywele.


Jino la tembo/mafuta ya nazi


Chukua vipande vya jino la ndovu, chemsha ndani ya mafuta ya nazi hadi kuyeyuka. Paka mchangayiko huo kichwani ili kuhamasisha uoteshaji wa nywele zilizonyonyoka.


Mada hii imeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment