Tuesday, 27 February 2018

Nyoka mwenye sumu kali agunduliwa ndani ya mkebe wa chakula cha mtoto


Nyoka mwenye sumu kali aliyegundulika ndani ya mkebe wa chakula cha mtoto

MWANAMKE amegundua nyoka mwenye sumu kali ndani ya mkebe ambao mtoto wake anatumia kebeba chakula cha mchana nchini Australia.
Nyoka huyo amegunduliwa amejificha kwenye kifuniko wakati mama huyo alikuwa akiweka chakula kwenye mkebe huko Adelaide, kulingana mshikaji nyoka Rolly Burrel.
Burrel amesema alimshauri mwanamke huyo kufunika mkebe na kuupeleka nje wakati alipompigi simu kumuomba usaidizi.
Alimtaja nyoka huyo kama eastern brown, mmoja wa nyoka wenye sumu kali zaidi duniani.
"Sio kitu ambacho ungetaka kukiona wakati ukiangalia kama mtoto wako kwa kweli alikula chakula chake," Burrel aliandika kwenye Facebook.
Amesema nyoka huyo alitolewa salama.
"Ni bahati sana kuwa alimuona nyoka huyo kwa sababu mtoto hata hawezi kuhisi akiumwa na kitu kidogo," aliiambia BBC.
Mshikaji nyoka huyo alisema kuwa anashuku nyoka huyo aliiangia kwennye mkebe huo kwa sababu labda ndiko alipata giza.
Nyoka wa aina hiyo hupatikana maeneo ya pwani mwa Australia na amehusika na vifo 23 tangu mwaka 2000 kwa mujibu wa utafiti.No comments:

Post a Comment