Tuesday, 27 February 2018

RPC Arusha anusurika katika ajali


Gari alilopanda Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo ambalo lilipata ajali jana

Wankyo Gati, ARUSHA

KAMANDA wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amenusurika kufa baada ya kupata  ajali eneo la Mdori mkoani Manyara.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo,  kaimu kamanda  wa polisi  mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 10 alasiri wakati kamanda Mkumbo akitokea mkoani Singida akiwa kwenye gari ya polisi lenye namba za usajili PT 2040.

Amesema licha ya kamanda Mkumbo wengine waliopata majeraha kidogo ni dereva na mlinzi wake ambao hakuwatajwa majina yao.

“Ni kweli Kamanda Mkumbo dereva wake pamoja na msaidizi wake  walipata ajali eneo la Mdori jana ya saa 10 jioni wakitokea mkoani Singida,”amesema.

Kwa mujibu wa Kamnada Ilembo dereva alikuwa anaendesha gari mwendo wa kawaida lakini kwa bahati mbata gari hilo lilipasuka gurudumu la nyuma na kusababisha gari hilo kuacha njia na kupinduka mara kadha.


No comments:

Post a Comment