Saturday, 10 February 2018

Serikali kuendelea kuagiza mataluma nje ya nchi
Jesca Kishoa


MBUNGE wa viti Maalum, Jesca Kishoa (Chadema) ameitaka serikali iseme ni kwanini inatumia fedha nyingi za kigeni kununua taaluma za kujengea reli  wakati  kuna mradi wa mkaa wa mawe ya mchuchuma na Liganga.

Hoja ya mbunge huyo ameitoa bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza ambapo alitaka kujua ni kwa nini  serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi za kigeni kuagiza mataaluma kwa ajili ya ujenzi wa Reli wakati kuna uwezekano wa kutumia chuma kutoka Mchuchuma na  Liganga.

Awali katika swali la msingi la mbunge wa Ludewa, Deogratias Ngalawa (CCM), alitaka kujua  ni lini mradi wa mkaa wa Mawe ya Mchuchuma na Chuma Liganga utaingizwa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/2021.

Pia alitaka kujua ni lini serikali italipa fidia kwa wananchi wa Mundidi na Mkomang’ombe waliotoa maeneo yao kupisha mradi.

Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Mhandisi Stella Manyanya amesema katika mradi wa ujenzi wa reli unaoendelea hauwezi kusubiri chuma kinachotengenezwa Mchuchuma na Liganga.

Amesema mataaluma yanayotumika katika ujenzi wa reli  ni yale ya chuma imara zaidi tofauti na chuma kinachozalisha hapa nchini hivyo uagizaji wa mataluma ya ujenzi wa reli utaendelea.

Aidha, amesema serikali inafanya utaratibu wa kufanya mazungumzo kupitia sheria mbalimbali zinazokinzana ili kuangalia maslahi mapana kwa taifa pamoja na wananchi wa Ludewa.No comments:

Post a Comment