Monday, 26 February 2018

Sugu ahukumiwa kwenda jela kwa kumtusi Rais Magufuli

     Joseph Mbilinyi al-maarufu Sugu

MBUNGE wa Mbeya mjini , Joseph Haule Mbilinyi al-maarufu kama Sugu (Chadema) na Katibu wa chama hicho kanda ya nyanda za juu kusini, Emmanuel Masonga wamehukumiwa kifungo cha miezi mitano gerezani.
Wawili hao walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

Mahakama imetoa uamuzi huo leo Jumatatu, Feb. 26, 2018 na hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mkoa wa Mbeya, Maiko Mteite,  baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa mashtaka.

Pia mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha miezi mitano Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,  Emmanuel Masonga,  kwa kosa hilo.

Washtakiwa hao wanatajwa kutenda kosa hilo Desemba 30, 2017 katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya wakati wakiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara.


No comments:

Post a Comment