Tuesday, 27 February 2018

Tamaa ya madaraka chanzo cha mauaji nchini- AskofuMary Meshack, Dodoma

ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kiluther  Tanzania -KKKT-  Dayosisi ya Dodoma,  Amon Kinyunyu amesema mauaji  yanayotokea katika jamii yanasababishwa  na  tamaa ya madaraka na watu kutopenda mabadiliko.

Ametoa kauli hiyo wakati akihubiri katika Ibada ya uwekaji wa jiwe la msingi  kwenye Kanisa la  Kiinjili la Kiluther Tanzania Usharika wa Nkuhungu mkoani hapa linalokadiriwa kutumia  zaidi ya milioni 826 .

Askofu Kinyunyu  amesema kama jamii itaendelea kuwa na uchu wa madaraka hakutakuwepo na maendeleo kwa kuwa baadhi ya watu wana tamaa ya madaraka.

Akizungumzia upande wa serikali amesema Dodoma sasa ni makao makuu ya nchi hivyo ni jukumu la waumini wote na jamii kwa ujumla kubadilika ili kuendana na kasi ya serikali ya Awamu ya Tano  ya kuleta mabadiliko katika mkoa wa Dodoma.


No comments:

Post a Comment