Saturday, 17 February 2018

Tambua nguvu ya tangawizi na msubili kwa tiba ya matubwitubwi
MATUBWITUBWI ni ugonjwa wa kuambukiza ambapo mgonjwa  anavimba mashavu hadi chini ya taya. Mara nyingi ugonjwa huu huwapata watoto wenye umri wa kati ya miaka mitano hadi 15.

Matubwitubwi husababishwa na virusi vinavyoshambulia vijifuko vya kutengeneza mate na mara chache sehemu nyingine za mwili.

Mgonjwa anaposhambuliwa na virusi hivi, huvimba sehemu ya chini za mashavu na wakati mwingine mashavu yenyewe. Mara nyingi uvimbe wake unaambatana na maumivu makali.

Si rahisi mgonjwa kuugua tena ugonjwa huu akishaupata mara moja, chanzo chake ni kula vyakula visivyostahili.

Tangawizi na msubili ni miongoni mwa dawa nzuri zinazoweza kusaidia kukomesha tatizo hili.

Tangawizi
Unga wa tangawizi kijiko kimoja cha chai, changanya na maji kidogo ili kupata uji mzito, upake sehemu zote za uso zilizovimba kwa uji huo hadi ukaukie sehemu za uvimbe.

Baada ya saa moja na nusu osha, fanya hivyo mara tatu kwa siku, kwa maana ya asubuhi, mchana na jioni kwa muda wa siku tatu hadi tano.


Msubili
Kata kipande cha msubili, parua upande mmoja halafu kipashe moto kisha nyunyizia unga wa bizari sehemu iliyoparuliwa na funga sehemu iliyovimba.

 Endelea na matibabu haya, yanafaa kufanywa wakati wa usiku na endelea nayo katika kipindi cha siku tatu hadi tano.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment