Tuesday, 6 February 2018

Tsvangirai mahututi
Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa (kulia) akipeana mkono na Morgan Tsvangirai mapema mwezi uliopita alipokwenda kumjulia.HALI ya afya ya kiongozi wa chama cha upinzani MDC nchini Zimbabwe, Morgan Tsvangirai inadaiwa kuwa yu mahututi katika hospitali moja nchini Afrika Kusini.

Vyanzo vya habari kutoka familia yake vinasema Tsvangirai (65), anatibiwa saratani ya utumbo na kwamba anakabiliwa na upungufu wa uzani, kuchoka na mishipa yake ya damu kuwa membamba.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema wakati wa harakati zake dhidi ya aliyekuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe , aliwahi kupigwa na kufungwa jela mara kadhaa.

Amekuwa akipelekwa hospitalini mara kwa mara tangu mwezi Juni mwaka jana, kupatiwa matibabu katika hospitali moja ya saratani mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Taarifa kutoka katika familia yake kupitia mtandao wa Bulawayo24  zinasema afya ya Tsvangirai ilidhoofika ghafla jana. Alipoteza hamu ya kula na akawa na tatizo kubwa la kushindwa kula wala kumeza maji.

Tsvangirai pia ameripotiwa kuwa na tatizo la kupumua.Wakati huohuo Duru za MDC zimesema Tsvangirai yuko mahututi na kwamba watu wanafaa kutarajia lolote wakati wowote.

Msemaji wa kiongozi huyo, Luke Tamborinyoka amesema kiongozi huyo wa MDC yuko hali nzuri lakini taifa linafaa kumuombea. Hata hivyo, hospitali ambayo Tsvangirai anatibiwa haijatoa tamko lolote kuhusu suala hilo.

No comments:

Post a Comment