Tuesday, 27 February 2018

Tumia dawa hizi kwa uzazi wa mpango
UZAZI wa mpango au wa majira ni muhimu ili kulinda afya ya mzazi pamoja na mtoto au watoto. Kuna njia kadhaa asilia zinazoweza kutumiwa bila kuathiri afya ya mama.

Njia hizo ni pamoja na matumizi ya mbegu za nyonyo, mbegu za embe, mdalasini, mzunguko wa hedhi na mnanaa.

Mbegu za nyonyo
Uchunguzi uliofanywa huko India unaonesha kuwa mwanamke anapotoka hedhini akitafuna mbegu moja ya nyonyo hatapata mimba mwezi huo.

Na kama hajataka kupata mimba aendelee mwezi wa pili, wa tatu na hata wanne. Wakati atakapohitaji kupata mimba inabidi akae mwaka mzima bila kutumia kinga hii.

Mbegu za embe na mdalasini
Chukua mbegu ya embe ponda hadi iwe uji, nusu saa kabla ya tendo la ndoa, weka kijiko kimoja cha chai cha uji huo katika sehemu ya uzazi, osha kabla tu ya tendo hilo na weka tena baada ya tendo hilo.

Siku moja baada ya kuzaa, tafuna kipande cha mdalasini kila jioni kwa muda wa mwezi mmoja kwa kufanya hivyo kipindi cha kuingia hedhini huahirishwa kwa muda wa miezi 15 hadi 20 ambapo mama hawezi kupata mimba.

Mzunguko wa hedhi

Mzunguko wa hedhi kwa wanawake wengi ni kati ya siku 21 hadi 30, kwa sababu haitakuwa rahisi kuzungumzia mizunguko yote, kinga inayotolewa hapo ni kwa mzunguko wa hedhi wa kati ya siku 28 na 30.
Ni vema hesabu kuanzia siku unapoingia hedhini, jizuie kufanya tendo la ndoa katika siku ya 11 hadi 18 ambazo ndizo za hatari. Siku nyingine zote hazina hatari labda itokee bahati mbaya.

Mnanaa

Kausha majani ya mnanaa kwenye kivuli, yasage na kuwa unga laini ambao utunze ndani ya chupa iliyo na mfuniko.
Kama kinga ya mimba, chukua vijiko viwili vya mezani vya mnanaa, koroga ndani ya glasi moja ya maji moto, baada ya kupoa kunywa nusu kabla ya tendo la ndoa.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa yeyote mwenye tatizo la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili na kuuepusha na magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment