Monday, 26 February 2018

Tumia hivi kukabili wingi wa damu ya hedhi


KIPINDI cha hedhi ni kati ya siku tatu hadi saba. Siku mbili za kwanzadamu hutoka kwa wingi na baadaye huanza kupungua na hatimaye kuacha.

Iwapo katika siku zote za hedhi damu itatoka kwa wingi na ikaendelea kutoka kwa siku zaidi bila kuonesha hali ya kuacha basi lazima kuwe na tatizo linalohitaji kupatiwa ufumbuzi.

Wakati mwingine hedhi inaweza kuja mapema sana au katika muda uliotarajiwa, hii pia inaonesha kwamba kuna tatizo ambalo linahitaji uchunguzi.

Hata hivyo, iwapo utabainika tatizo kuna tiba za mimea na matunda ambazo zinaweza kusaidia kuondokana na hali inayokusumbua ambazo ni pamoja na komamanga, maua ya mgomba, karoti na bitiruti, gome la mwembe na giligilani.

Komamanga

Tengeneza glasi moja ya juisi ya komamanga kunywa kila asubuhi wakati wa kifungua kinywa. Anza tiba siku tatu kabla ya muda wa hedhi kama tatizo hilo lilishatokea siku za nyuma au anza tiba utakapogundua kwamba tatizo hilo limeanza. Endelea nayo hadi siku mbili zaidi baada ya damu kuacha.

Karoti/bitiruti

Tengeneza glasi moja ya juisi kwa kutumia kiasi sawa cha bitiruti na karoti, kunywa kila siku kwa muda wa vipindi viwili vya hedhi (miezi miwili)

Gome la mwembe

Tengeneza juisi ya gome bichi la mwembe, kunywa glasi moja,  na nusu yai lililopikwa, kila jioni na asubuhi katika kipindi chote cha hedhi. Endelea siku mbili baada ya damu kuacha kutoka.

Giligilani

Chukua kijiko kimoja cha mezani cha mbegu za giligilani weka ndani ya nusu lita ya maji, chemsha hadi maji hayo yabaki yakiwa nusu mililita 250.

Chuja na kunywa maji hayo yakiwa bado yana hali ya uvuguvugu. Endelea na tiba hii kila siku kwa kipindi chote cha hedhi na siku mbili baada ya damu kuacha kutoka.

Maua ya mgomba

Pika ua moja la mgomba, kula pamoja na glasi moja ya mtindi, fanya matibabu asubuhi na jioni kila siku hadi damu zitakapokuwa zimeacha kutoka. Endelea na tiba hii kwa siku mbili zaidi.

Mada hii imeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wasiliana na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment