Tuesday, 6 February 2018

Tumia hivi kumaliza tatizo la kikojozi kwa mwanao
KUKOJOA kitandani ni tatizo lililozikumba  baadhi ya familia baada ya mtoto au watoto wao kukabiliwa nalo.

Kimsingi mtoto anatarajiwa kuacha kukojoa anapofikisha umri wa miaka miwili hadi mitatu. Baada ya umri huo linakuwa tatizo linalohitaji kutatutiwa.

Uzoefu unaonesha kuwa moja ya sababu inayochangia tatizo hilo ni michezo mingi ya mtoto wakati wa mchana ambapo usiku ana  lala bila kujitambua.

Hata hivyo, zipo tiba zinazosaidia mtoto kuachana na hali hiyo kabisa.

Miongoni mwazo ni pamoja na asali, ufuta mweusi, ndevu za mahindi na vitungu maji vilivyochanganywa na asali.

Asali
Chukua kijiko kimoja cha mezani cha asali mlambishe mtoto polepole hadi amalize kabla ya kwenda kulala. Tiba hii ni ya mwezi mmoja hivyo mzazi jitahidi kufanya hivyo kila siku.

Ufuta mweusi
Chukua kijiko kimoja cha mezani cha ufuta mweusi, saga kisha changanya na sukari guru kiasi kinacholingana, mpe mtoto ale kabla ya kwenda kulala. Endelea na tiba hiyo kwa muda wa mwezi mzima.

Ndevu za mahindi
Chukua ndevu za mahindi saba chemsha na glasi mbili za maji, mpe mtoto anywe kabla ya kwenda kulala. Endelea kumpa kwa kipindi cha mwezi mzima.

Vitunguu maji/asali
Ni vema uchukue kitunguu maji saga kiwe ujiuji, chukua kijiko kimoja cha mezani chenye ujiuji huo changanya na  kingine chenye asali, mpe mtoto atumie mchanganyiko huo kutwa mara tatu kwa muda wa siku 30.
No comments:

Post a Comment