Wednesday, 21 February 2018

Tumia hivi vinasaidia kutibu tatizo la kuuma na kutotoka mkojo Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai akizungumzia nguvuya iriki, dafu na radishi kwa tiba ya mkojo kuuma na kutotoka.
MKOJO ni sehemu muhimu ya utoaji wa taka mwilini. Kazi yake kubwa ni kuondoa maji ya ziada na uchafu unaojichanganya baada ya damu kuchujwa na figo.

Baadhi ya watu  wakati wa baridi wanapokwenda kukojoa mishipa husinyaa na mkojo hutoka katika matone na kwa maumivu yanayosababishwa na kupanuka kwa kibofu cha mkojo kutokana na wingi wake.

Ugonjwa huo kama yalivyo magonjwa mengine yanatiba inayoweza kumsaidia mtu kuondokana na hali hiyo, tatizo la kuuma na kutotoka kwa urahisi mkojo linatibika kwa kutumia iriki na maziwa, radishi, dafu na giligilani.

Iriki/maziwa

Chukua kijiko cha chai cha unga wa iriki, changanya na nusu glasi ya maziwa, kunywa kila siku asubuhi kabla ya kufungua kinywa kwa chakula au kinywaji kingine chochote. Endelea na tiba hii kwa muda wa mwezi mmoja utaondokana na hali hiyo.

Radishi

Chukua radishi nne katakata vipande vidogo vidogo, kula polepole ukitafuna kikamilifu kwa muda wa dakika tano hadi 10. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku 20 utaona nafuu kwa kiwango kikubwa.

Dafu

Kunywa glasi mbili za maji ya dafu kila siku kwa muda wa siku 20, utaondokana kabisa na hali hiyo au kupata nafuu kwa kiasi kikubwa.

Giligilani

Loweka vijiko viwili vya mezani vyenye giligilani katika glasi ya maji kwa muda wa saa 12, kisha ziponde zikiwa ndani ya hayo maji kisha chuja na kunywa maji yote. Tumia dawa hiyo kila siku kwa muda wa siku 14.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la kiafya, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa. Tunatumia virutubisho vinavyotokana na mimea kwa tiba yenye uhakika.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.No comments:

Post a Comment