Friday, 9 February 2018

Ufahamu Mwifa suluhisho la maradhi ya ngiri

NGIRI au Hernia ni ugonjwa unaompata  mtu baada ya misuli au kuta za tishu zinazoshikiria au kubeba viungo vya mwili kupoteza uimara wake.

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni pamoja na tumboni, eneo la kinena, kwenye  paja upande wa juu, shingoni na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji.

Tatizo hilo huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kusababisha mtu apate  ngiri ni uzito mkubwa wa mwili au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu.

Ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua pia yanasababisha misuli au tishu kupoteza uimara au uwazi na hivyo kumsababishia ngiri.

Tiba ya ngiri ni kufanyiwa upasuajia ili kurekebisha misuli au tishu zilizolegea lakini ushauri wangu, ni vema mtu afanye mazoezi ili kupunguza uzito pamoja na kuweka utaratibu mzuri wa kula chakula kinachojumuisha mboga za majani na matunda yenye nyuzi nyuzi ambavyo vinasaidia mmeng’enyo wa chakula tumboni na kuepusha kuvimbiwa.

kula matunda  kuna faida kubwa kwa kuwa yana wingi wa vitamini C ambayo husaidia kuunganisha tishu zilizolegea na kuponyesha haraka kwa sehemu iliyofanyiwa upasuaji.

Na kama tatizo lako ni la kukohoa kwa muda mrefu kunakosababishwa na uvutaji wa sigara, ni vema ukasitisha uvutaji ili kupunguza madhara au makali ya ngiri lakini pia kusitisha sigara kwa ajili ya usalama wa afya yako.

Hata hivyo, Kampuni yetu ya virutubisho tiba (Mandai Products Company) imegundua kirutubisho Mwifa ambacho kina uwezo wa kusaidia matatizo ya ngiri, tumbo na kuongeza hamu ya kula.

Kirutubisho hiki kinaimarisha kinga ya mwili na kuufanya kutoshambuliwa na magonjwa kirahisi kwa kuwa kimeandaliwa kwa ufanisi mkubwa kwa kutumia mimea tiba.

Kwa yeyote anayesumbuliwa na tatizo la  ngiri anaweza kuja makao makuu yetu Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia dawa hii.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255716 300 200, +255784 300 300, +255769 400 800  au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufuatilia makala zake kupitia Gazeti TAMBUA kila JUMATATU.

No comments:

Post a Comment