Saturday, 10 February 2018

Uhakiki madeni; Serikali yaokoa bilioni 84 za watumishi hewa, vyeti feki                                       Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango

WATUMISHI wa Serikali 82,111 waliokuwa wakiidai serikali kwa zaidi ya miaka 10 watalipwa madeni yao sanjari na mshahara wao wa mwezi Februari.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk.Philipo Mpango ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari.

Waziri Dk. Mpango amesema madai ya watumishi yana thamani ya shilingi bilioni 43.39 huku mengine yana zaidi ya miaka 10, na kwamba majina ya walipwaji wote yatatangazwa kwenye magazeti.

Dk. Mpango amesema baada ya uhakiki Serikali kupitia mfumo wa taarifa za kiutumishi na mishahara, hadi kufikia Julai Mosi mwaka jana ilikuwa na madai ya mishahara yenye thamani ya sh, bilioni 127.6 kwa watumishi 82,111.

Amebainisha kuwa kati yao walimu ni 53,925 ambao wanadai sh. bilioni 53.9 ambayo ni sawa na asilimia 42.27 ya madai yote na wasiokuwa walimu 8,186 waliokuwa wakidai sh. bilioni 73.6 sawa na asilimia 57.7
ya madai yote.

Amesema madai hayo yalikuwa ya muda mrefu mengine yakiwa ya kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2017.

Waziri huyo amesema madai hayo yalijumuisha mishahara isiyolipwa, tofauti ya mishahara kutokana na kukaimu na nyongeza za mishahara zilizotokana na kupandishwa na kuchelewa kurekebishiwa mishahara.

Dk. Mpango ametanabaisha madai ya watumishi 27,389  kati ya 82111 yenye jumla ya sh. bilioni  43.39 ikiwa ni sawa na asilimia 34 ya madai yote ya sh. bilioni 127.6 yaliyohakikiwa yameonekana ni sahihi na kulipwa bila marekebisho.

Amesema madai yanayostahili kulipwa yanajumuisha sh. bilioni 16.25 kwa walimu 15,919 na sh. bilioni 27.15 kwa watumishi wasiokuwa walimu 11,470
.
Amezidi kufafanua kuwa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara, watumishi hewa, vyeti feki na wasiokuwa na sifa na uhakiki kwa madai ya malimbikizo ya mishahara uliofanyika limeweza kuokoa sh. bilioni  84.22 ambazo ni sawa na asilimia 66 ya malimbikizo ya awali.No comments:

Post a Comment