Monday, 19 February 2018

Unaweza kukabiliana na kichomi kwa kufanya haya
Mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai akifafanua njia ambazo jamii inaweza kutumia kukabiliana na kichomi.


MARADHI ya kichomi yanasababishwa na hitilafu katika mapafu baada ya viungo hivyo kushambuliwa na wadudu.

Mara nyingi matokeo ya matatizo haya huwa ni homa kali, maumivu makali ya kifuani, kupumua kwa shida wakati mwingine hali hiyo inaweza kuambatana na kikohozi chenye makohozi.

Maradhi haya yanaweza kutibiwa kwa vyakula vyetu tunavyovitumia kila siku ambavyo ni pamoja na kitunguu swaumu, methi, karoti, spinachi na tango.

Kitunguu swaumu
Namna ya kuandaa tiba hii, chukua punje 10 za kitunguu swaumu ziponde na kuwa katika hali ya ujiuji, ongeza maziwa robo glasi na asali kijiko kimoja cha mezani changanya vizuri mpe mgonjwa anywe.

Kama tiba ya ziada, paka kitunguu swaumu katika sehemu zenye maumivu, endelea na tiba hii asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba.

Methi
Hii ni aina ya mboga inayopatikana katika masoko ya mboga hasa kwa ajili ya watu wenye asili ya kihindi.

Hakikisha kichomi kinapoanza tu, tengeneza chai iliyokolea methi, kunywa vikombe vinne kwa siku bila kutumia chakula cha aina yoyote  isipokuwa maji tu.

Ili kuboresha ladha ya chai ya methi, unaweza kukamulia maji ya limau. Endelea na tiba hii kwa muda wa siku tatu.

Karoti, spinachi na tango
Tengeneza mililita 200 za juisi ya spinachi, changanya na mililita nyingine  100 za juisi ya tango na nyingine 300 za juisi ya karoti. Kunywa mchanganyiko wote huo kwa mara moja. Tiba hii ifanyike asubuhi na jioni kwa muda wa siku saba.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa Tiba, Lishe na Virutubisho, Abdallah Mandai.

Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam wetu kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.


No comments:

Post a Comment