Saturday, 24 February 2018

Undongo mweusi unavyotibu yutikaria

Udongo mweusi


YUTIKARIA ni ugonjwa wa kuwashwa na kuwa na uvimbe mwili mzima. Mara nyingi ugonjwa wa aina hii ni dalili ya mzio.

Mwathirika anapata uvimbe ghafla na kuwashwa na kisha hali hiyo huweza kutoweka ghafla licha ya kuwa wakati mwingine inaweza kudumu kwa muda mrefu na hivyo kuhitaji tiba.

Zipo tiba nyingi za asili miongoni mwanzo ni udongo mweusi, tui la nazi na mtindi, maji ya mchele, ndimu, asali na bizari.

Udongo mweusi

Paka udongo mweusi mwili mzima na baada ya saa moja oga ili kuondoa udongo wote

Tui la nazi

Baada ya kuoga, paka tui la nazi au mtindi mwili mzima. Baada ya saa moja oga mwili mzima.

Maji ya mchele

Pia unaweza kunywa maji yaliyooshewa mchele, asubuhi na jioni kwa muda wa siku tatu. Hakikisha maji uliyoshea ni safi na salama.

Ndimu na asali

Changanya juisi ya ndimu na asali, ongeza maji ya kawaida nusu glasi, halafu kunywa. Fanya hivyo asubuhi na jioni kwa muda wa siku tatu.

Bizari

Kula kikonyo kimoja cha bizari kila siku asubuhi, kabla ya kupata kifungua kinywa kwa muda wa siku tano.

Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho,  Abdallah Mandai.

Yeyote anayesumbuliwa na tatizo la kiafya na ushauri, karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri na kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili dhidi ya magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.
 

No comments:

Post a Comment