Saturday, 24 February 2018

Vikwazo vizito zaidi dhidi ya Korea Kaskazini vyawekwa na Marekani


 Donald Trump


WAZIRI wa Fedha wa Marekani, Steve Mnuchin ameyaonya mataifa yanayoshirikiana kibiashara na Korea Kaskazini kwamba yanafanya hivyo yakijihatarisha yenyewe.

Akitangaza vikwazo vipya Mnuchin amesema kampuni yoyote iliyosaidia kufadhili mpango wa kinyuklia wa Pyeonyang itapoteza haki ya kufanya biashara na Marekani.
Pia amesema Marekani sasa huenda ikaanza kupanda na kuchunguza meli zinazo safirisha mizigo Korea Kaskazini.
Vikwazo hivyo vinalenga mabenki na kampuni zinazomiliki meli ambazo Marekani inasema zinafanya biashara na Korea Kaskazini.
Rais Trump aliviitaa vikwazo hivyo vizito zaidi, lakini waandishi wanasema vilivyowekwa hapo awali vililenga mitandao ya kibiashara ya Korea Kaskziniu.
Vikwazo hivyo vinalenga zaidi ya meli 50, kampuni za uchukuzi nchini Korea Kaskazini lakini pia China na Taiwan.
Korea Kaskazini inakabiliwa na vikwazo vya kimataifa pamoja na vile vya Marekani kuhusu mpango wake wa Kinyuklia.
Lakini taifa hilo liliendeleza majaribio ya makombora yake mwaka uliopita ikiwemo majaribio ya silaha za kinyuklia mbali na kombora la masafa marefu linaloweza kufika Marekani.
Marekani inasema vikwazo hivyo vipya vinalenga kuifinya zaidi Korea Kaskazini kupitia kukata vyanzo vyake vya fedha na mafuta ili kutoendeleza mpango wake wa Kinyuklia.
Idara ya fedha ya Marekani imeorodhesha kampuni 16 hususan za meli zilizopo nchini Korea Kaskazini, lakini tano zimesajiliwa Hong Kong, mbili China, nyingine idadi hiyo Taiwan moja Panama na nyingine moja Singapore.
Meli 28 zimeorodheshwa katika orodha hiyo nyingi zikitoka Korea Kaskazini lakini mbili zina bendera ya Panama moja kutoka Comoros na nyingine iliyo na bendera ya Tanzania.
Akizungumza katika mkutano na vyombo vya habari leo, Trump ameonya dhidi ya hatua kali iwapo vikwazo hivyo havitazaa matunda.
“Iwapo vikwazo hivyo havitafanya kazi tutaingia katika awamu ya pili ambayo itakuwa kitu kibaya pengine kibaya sana kwa ulimwengu.
“Ni taifa lisiloaminika na lisilofuata kanuni, iwapo tutakubaliana itakuwa kitu kizuri na iwapo haitawezekana kitu kitafanyika,”amesisitiza Trump.
Hata, hivyo hakuelezea zaidi ni hatua ghani zitakazochukuliwa katika awamu ya pili.
Marekani imekuwa ikiuwekea utawala wa taifa hilo vikwazo tangu mwaka 2008 na kwamba vikwaza hivi vipya vinatanguliwa na vingine vilivyowekwa Novemba mwaka jana ambavyo vililenga meli za Korea Kaskazini pamoja na kampuni za China zinazofanya biashara na Pyongyang.
Umoja wa mataifa ulifuata nyayo hizo baada ya kuwekewa vikwazo vingine vilivyoungwa mkono na mataifa 15 wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo hatua za kukatiza uagizaji wa mafuta kuingia Korea Kaskazini kwa silimia 90.No comments:

Post a Comment