Friday, 23 February 2018

Wabunge Kenya wajadili bungeni ukosefu wa karatasi za kwenda haja kubwa                 Bunge la Kenya


WAKENYA wamewataka wabunge wao kubeba karatasi zao za kutumia baada ya haja kubwa bungeni iwapo wameghadhabishwa na ukosefu wa karatasi hizo bungeni.

Wabunge katika mjadala siku ya Jumatano walitumia muda wao mwingi kulalamikia ukosefu wa karatasi hizo na maji katika vyoo vyao.
Ni suala lililowaunganisha wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani. Kiongozi wa walio wachache bungeni John Mbadi amesema sio maji pekee ambayo hakuna bali hata karatasi hizo.
“Huwezi kuniambia kwamba bunge ambalo wabunge wa taifa wanafanya kazi zao halina karatasi za kwendea haja kubwa na kwamba mara nyingine unaingia chooni na hakuna karatasi hizo,”amesema Mbadi.
Mbadi aliongezea kuwa suala hilo la choo ni tete mno huku mifereji pia ikikosa maji hivyo kuwa vigumu kwa wabunge kutekeleza wajibu muhimu wa kuwa wasafi.
Mwanzo katika jumba la Continental unafaa kuwa makini sana , unafaa kuangalia iwapo kuna maji kwa sababu unaweza kujichafua....kabla ya kuchukua hatua yoyote ni lazima uhakikishe kwamba kuna maji katika mifereji. Kwa sababu unahitaji maji hayo baada ya kufanya mambo fulani'', aliongezea Mbaddi.
Kiranja wa walio wachache bungeni ambaye pia ni mbunge wa Suna Mashariki, Junet Mohammed aliishutumu kamati ya maandalizi katika bunge la 11 kwa kushindwa kuimarisha hali ya wabunge licha ya kusafiri katika mataifa kadhaa ikiwemo Uganda ili kujifahamisha.

alio wachache bungeni ambaye pia ni mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed aliishutumu kamati ya maandalizi katika bunge la 11 kwa kushindwa kuimarisha hali ya wabunge licha ya kusafiri katika mataifa kadhaa ikiwemo Uganda ili kujifahamisha.
''Bwana Spika chai inayotolewa hapa haina maziwa na inafanana na ile inayotolewa wakati wa matanga'', amesema katika matamshi yaliozua kicheko kutoka kwa wabunge wenzake.
Mbunge wa Nambale Sakwa Bunyasi alisema bunge halihitaji wapishi pekee bali wapishi wataalam ambao wanaweza kupika vyakula vizuri.
Naye naibu kiongozi wa walio wengi bungeni, Jimmy Angwenyi alisema kuna umuhimu wa idara ya upishi kuimarisha upikaji wa vyakula.
''Naamini kwamba tuliwaajiri watu wanaofaa kupika chakula kizuri. Sifai kupiga foleni kwa muda mrefu kwa sababu mimi ni mzee naweza kuzirai''.
''Bwana Spika sio haki kwamba baadhi ya maeneo ya kuegesha magari waliyotengewa wabunge yamechukuliwa na maofisa wengine, hatuwezi kuingia katika eneo la kufanyia mazoezi tunapohitaji,'' alisema Angwenyi.
Chanzo BBCNo comments:

Post a Comment