Monday, 26 February 2018

Wacheza utupu wanavyohudhuria mazishi China
KATIKA baadhi ya maeneo hususan vijijini nchini China wacheza utupu wamekuwa wakicheza densi na umati ukishangilia. Unaweza kuliona hilo wakati wa mazishi.
Mapema mwaka huu, China ilianza tena kuwakamata wacheza utupu wanaocheza densi kwenye mazishi, harusi na mahekalu.
Hiyo siyo mara ya kwanza mamlaka zimejaribu kuzuia tabia hizo lakini bado hazijanafikiwa. Imani nyingine zinasema kuwa suala hilo ni la kuabudu.
Wacheza utupu hao hutumiwa kuwavutia watu wnaaohudhuria mazishi kwa sababu uwepo wa watu wengi huonekana kama heshima kwa marehemu.
Hata hivyo, imani nyingi ni ile kuwa kuwaajiri wacheza utupu kunaweza kuonekana kama ishara ya utajiri.
Maeneo ya vijijini nchini China ndiyo yenye tabia ya kutumia fedha nyingi hata kuliko mapato, kuwalipa waigizaji, waimbaji, wachekeshaji na wacheza utupu kuwatumbuiza wale waliofiwa.
Tamaduni hiyo inapatikana sana maeneo ya vijijini ya China na ni maarufu zaidi nchini Taiwan ambapo ilianzia.
"Tamaduni hii ya wacheza utupu kwenye mazishi kwanza ilipata umaarufu nchini Taiwan mwaka 1980," msomi wa chuo cha South Carolina Marc Moskowitz aliiambia BBC.
Tamaduni hii imepata umaarufu nchini Taiwan lakini nchini China serikali imeizuia na watu wengi hawafahamu kuihusu.No comments:

Post a Comment