Thursday, 8 February 2018

Waijua Kabliti? Itumie sasa kiboko ya mapunye
MAPUNYE ni fangasi wanaoshambulia eneo la kichwa pekee ukiacha lile la usoni. Kwa maneno mengine, aina hii ya fangasi haishambulii uso bali eneo lililobaki la kichwa.

Mapunye huwashambulia watu wa jinsia na umri wowote, ingawa huonekana zaidi kwa watoto wadogo.  Hushambulia watoto ambao hawajafikia umri wa balehe na mara nyingi huacha kushambulia pale mtoto anapofikia umri huo.

Ugonjwa huu unaweza kushambulia eneo zima la kichwa au sehemu tu. Wakati mwingine eneo la ngozi ya kichwa ambalo lina mashambulizi ya mapunye huwa na umbo linalofanana na sarafu.

Eneo lililoathiriwa na mapunye, nywele hunyonyoka na hivyo mwonekano wa mfano wa sarafu huonekana wazi hata bila kutumia jicho la kitaalamu.


Dalili za mapunye

Ukiachilia mbali mwonekano wa mapunye kama nilivyoeleza kuna dalili nyingine za maradhi hayo ambapo ngozi iliyoshambuliwa huwasha, ingawa si mara zote na kubadilika kwa rangi ya ngozi ya eneo lenye maambukizi.

Ukitazama kwa makini eneo ambalo lina mashambulizi ya maradhi hayo utagundua kuna vidoti vyeusi ambavyo vinaonesha eneo ambalo nywele zimeng'oka.

Dalili nyingine ya mapunye ni ngozi kubanduka kwenye eneo lenye maambukizi na pia ngozi kukauka kwenye eneo hilo. Mara nyingine usaha pia huweza kuonekana kwenye eneo la ngozi lililoshambuliwa na aina ya fangasi hao, hali hiyo kitaalamu inaitwa kerions.

Kama maradhi haya yakikaa bila kutibiwa kwa muda mrefu yanasababisha dalili nyingine ambayo ni kuonekana kama kutoka majimaji kwenye eneo la ngozi lililoathirika pamoja na kutoka harufu mbaya kwenye eneo hilo.

Watu ambao wako katika hatari ya kupata maambukizi ya mapunye ni wale wanaoshirikiana na wenzao vifaa vya kunyolea bila kuvisafisha vizuri.

Hata hivyo, Kampuni yetu ya virutubisho tiba (Mandai Products Company), imegundua kirutubisho Kabliti ambacho kinapatikana katika mfumo wa kimiminika na husaidia kuponyesha majeraha mapunye.

Bidhaa hii ni nzuri sana kwa matatizo ya ngozi licha ya kusaidia sana katika kutokomeza mapunye, Kabliti pia huondoa hali ya mwasho kwenye ngozi.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo la  mapunye anaweza kuja makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Abdallah Mandai kwa ushauri au kujipatia dawa hii.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255716 300 200, +255784 300 300, +255769 400 800  au barua pepe dkmandaitz@gmail.com. Pia unaweza kufuatilia makala zake kupitia Gazeti TAMBUA kila JUMATATU.

No comments:

Post a Comment