Wednesday, 28 February 2018

Wajawazito Ghana watumia vidonge vya kuwachubua ngozi watoto tumboniWANAWAKE nchini Ghana wameonywa kutotumia dawa za kujichubua ili kubadilisha ngozi ya watoto kuwa nyeupe wakati bado wako tumboni.
Wataalam wa afya wanasema dawa hizo haramu zinapelekea madhara ya uzazi ikiwemo viungo vya ndani vya mtoto kuharibika.
Mamlaka ya Vyakula na Dawa Ghana (FDA) imesema utumiaji wa vidonge vya Glutathione ni hatari ikiongezea kuwa inataka " umma ufahamu kuwa hamna dawa zilizoruhusiwa na FDA aina ya vidonge vya kuchubua ngozi ya mtoto aliye tumboni"
Vitendo vinashamiri nchini Ghana, kwa mujibu wa FDA, mara nyingi vidonge hivyo vinaingizwa kinyemela ndani ya mizigo kwa viwango vikubwa kupitia viwanja vya ndege.
Polisi na vikosi vya usalama wanafanya kazi pamoja kuwashika na kuzishtaki kampuni na watu binfsi watakaokuwa na vidonge visivyoruhusiwa.No comments:

Post a Comment