Wednesday, 28 February 2018

Wajui chumvi ni dawa ya mdudu wa sikio?


 Chumvi ambayo ndiyo tiba ya mdudu ndani ya sikio

MDUDU katika sikio ni tatizo ambalo humpata mwanadamu ghafla ambapo anahitaji pia tiba ya haraka ili kuondokana nalo.
Unapoona umepatwa na hali hiyo tumia chumvi au muarobaini kukabiliana na tatizo hilo.

Chumvi

Weka chumvi ndani ya maji vikisha changanyika weka ndani ya sikio lililoingiliwa na mdudu kisha ziba kwa pamba baadaye inamisha kichwa upande wa sikio ambapo maji na mdudu vitatoka pamoja.

Muarobaini

Tengeneza juisi ya muarobaini ichanganye na chumvi kisha weka matone matano hadi saba ndani ya sikio halafu lizibe kwa pamba. Kaa kwa muda fulani kisha ondoa pamba na inamisha sikio lenye mdudu kutoa juisi ambapo vitatoka na mdudu akiwa ameshakufa.


Mchanganuo huu umeletwa kwako na Mtaalamu wa tiba, lishe na virutubisho, Abdallah Mandai.

Kwa anayesumbuliwa na tatizo lolote la kiafya karibu makao yetu makuu, Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au awasiliane na Mtaalam Mandai kwa ushauri au kujipatia virutubisho mbalimbali vinavyoukinga mwili ili kuuepusha na magonjwa.

Mtaalamu Mandai anapatikana kwa simu +255745900600 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment