Tuesday, 27 February 2018

Walimu watakaojihusisha kimapenzi na wanafunzi kukiona


 Waziri wa Tamisemi Seleman Jaffo

Mary Meshack, Dodoma

WAZIRI wa nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jaffo amewataka maofisa elimu kote nchini kutowaficha waalimu wanaofanya  vitendo viovu dhidi ya wanafunzi.

Jafo ametoa kauli hiyo leo mjini Dodoma wakati akifungua kikao cha kazi cha maofisa elimu wa mikoa na wilaya na makao makuu ya wizara.

Amewataka maofisa elimu kuwabainisha walimu hao ili wachukuliwe  hatua za kisheria dhidi ya vitendo vyao viovu kwa wanafunzi.

“Kama walimu jukumu lao kubwa ni kusimamia nidhamu dhidi ya wanafunzi, lakini kuna baadhi yao wamekuwa wakikiuka maadili kwa kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi jambo ambalo linakiuka maadili ya kazi yao,”amesema Jafo.

Kutokana na mkoa wa Dodoma kutokuwa na historia ya kufanya vizuri katika sekta ya elimu, kupitia kikao hicho imemlazimu Waziri Jaffo kumwagiza Naibu katibu mkuu wa Tamisemi, Mhandisi Mussa Iyombe kuchunguza na kufanya maboresho ili mkoa huo ambao ndio makao makuu ya nchi ufanye vizuri.
  

No comments:

Post a Comment